The House of Favourite Newspapers

BENKI YA DUNIA YAIPIGA TAFU SWIOFISH PIKIPIKI 17 HALMASHAURI 5

0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk.Yohana Budeba akisoma hotuba yake.
Viongozi wa wizara hiyo wakifafanua jambo.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Baadhi ya Pikipiki zilizotolewa na Benki ya Dunia.

 

…Zoezi la kukabidhi pikipiki likifanyika.
Dk. Budeba akikabidhi pikipiki zilizotolewa.

 

BENKI ya Dunia (WB), imetoa msaada wa pikipiki 17 kwenye Halimashauri za wilaya tano, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kusaidia mradi wa SWIOFish unaojihusisha na uvuvi wa Bahari Kuu, kufuatia kujiridhisha na utendaji kazi wake katika Ukanda wa Pwani.

Akizungumza katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk.Yohana Budeba kwa niaba ya waziri wa wizara hiyo, Dk. Charles John Tizeba alitoa shukurani za dhati kwa Benki ya Dunia kujitolea msaada huo.

“Niwashukuru Benki ya Dunia kwa namna ya pekee, kwanza kuwa naimani na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi kufikia hatua ya kujitoa na kufadhili mradi huu ambao kwa kweli unayo manufaa makubwa mno kwa taifa, pikipiki hizi 17 ambazo thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 93, nami nazikabidhi kama zilivyo kwa halimashauri za wilaya teule,” alisema Dk. Budeba na kuongeza;

“Sekta ya Uvuvi ni miongoni mwa sekta muhimu za uzalishaji wa kiuchumi kwa ustawi wa maendeleo ya taifa letu, lazima tuipe kipaumbele stahiki kuhakikisha inasonga mbele kwa kiwango hitajika, maana idara ya uvuvi pekee huweza kutoa ajira za moja kwa moja kwa wananchi wapatao 183,200 na zaidi ya wananchi 4,000,000 hupata ajira kwa kujishughulisha na uvuvi kwa njia moja au nyingine, kwa hapo mnaweza kuona namna ambavyo sekta hii ina umuhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini,” alisema Dk. Budeba.

Aidha, alisema mbali na Benki ya Dunia, wizara kupitia sekta hiyo ya uvuvi imekuwa ikitafuta uwezeshaji wa miradi mbaliambali kupitia vyanzo tofautitofauti, ili kuwezesha ukuzaji na upanuaji wa miradi kama ile ya kikanda mfano, South West Indian Ocean Fisheries Governance And Shared Growth (SWIOFIsh) ambao unatekelezwa katika nchi tatu za Tanzania (Bara na visiwani), Msumbiji na Jamhuri ya Watu wa Congo.

“Tunaamini kwamba vikundi hivi vikisaidiwa na kusimamiwa ipasavyo vitaweza kushiriki kikamilifu katika suala zima la ulinzi wa rasilimali za uvuvi ikiwemo ukusanyaji wa takwimu za uvuvi ambazo ni kitovu cha upangaji wa mipango ya uvuvi endelevu katika kutekeleza sera ya mwaka 2015, hivyo tuungeni mkono harakati na jitihada zinazofanyika,” alimaliza Dk. Budeba.

Leave A Reply