The House of Favourite Newspapers

Benki ya NMB Wazindua Huduma Mpya

..Akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya huduma hizo mpya za benki.

 

Benki ya NMB mapema wiki hii walifanya uzinduzi wa huduma tatu mpya za Benki hiyo uliofanyika
Hoteli ya Hyatt hivi  karibuni na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya fedha, teknolojia na baadhi ya wateja wa NMB.

Huduma zilizozinduliwa ni uwezo wa mwananchi kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, App yenye huduma zote ambazo mteja anaweza kufanya mwenyewe badala ya kwenda kwenye tawi na Scan to Pay huduma ya kufanya malipo kwa kutumia QR code na hivyo kuwawezesha kulishikishwa kifedha.

 

App ya NMB KLiK inapatikana katika Playstore
https://goo.gl/Fr9fZf na kupitia AppStore https://goo.gl/wQXZV6

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Naibu Gavana Usimamizi wa Fedha Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) Dk.Benard Kibese ambaye alisema kwamba ubunifu huo utarahisha Watanzania
wengi kufungua akaunti za benki hiyo kupitia simu zao za mikononi na kwamba hivi sasa watumiaji
wa simu za mkononi ni wengi na hivyo huduma hiyo ya NMB imekuja wakati sahihi.

 

“Tunaipongeza NMB kwa ubunifu huu ambao wamekuja nao wa kuhakikisha wanatumia teknolojia
iliyopo kuanzisha huduma za kufungua akaunti kupitia simu ya mkononi na kizuri zaidi hata wenye
simu za tochi bado wanaweza kufungua akaunti kupitia huduma hiyo,” alisema Dk.Kibese.

Huduma hii imepokelewa vizuri na watumiaji wa mtandao wa Twitter ambao wamesema kwamba
uzinduzi huo ni muhimu sana hususani katika mchakato wa kuipeleka Tanzania katika Uchumi wa
kati.

Comments are closed.