Benki ya NMB kwa kushirikiana na Jukwaa la Kimataifa la Maziwa na wadau wengine wameungana kukutanisha wadau wa sekta ya maziwa ili kuangalia namna ya kukuza uzalishaji, uchakataji na matumizi maziwa hususani nchini Tanzania.
Wadau hao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali na Tanzania wanakutana kwa siku mbili mfululizo kuangalia namna bora ya kuifanya sekta ya maziwa kufanya vizuri zaidi na kushiriki katika kupunguza umasikini kwa jamii zinazozalisha bidhaa hiyo.
Benki ya NMB imetumia zaidi ya shilingi bilioni 100 kwa ajili ya mikopo kwa wakulima mbalimbali ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kuinua kilimo ikiwemo sekta ya maziwa nchini.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Luhaga Mpina akizindua mkutano huo leo jijini Dar es Salaam, aliishukuru NMB kwa kukutanisha wadau hao kujadili namna bora ya kuinua sekta hiyo nchini Tanzania.
Comments are closed.