The House of Favourite Newspapers

Benki ya NMB Yakabidhi Mabati ya Mil. 17- Kwa Shule Kisarawe

0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kushoto) akishukuru baada ya kukabidhiwa mabati 565 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (wa kwanza kulia) yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuezekea vyumba vya madarasa vya Shule tau za Kurui Chole, Msegamo na Kidugalo. Katikati ni Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Benedict Baragomwa na kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Dismas Prosper.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (kushoto) wakipiga makofi baada ya kupokea mabati 565 yaliyotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya kuezekea  vyumba vya madarasa vya shule za Kurui Chole, Msegamo na Kidugalo. Kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki, Dismas Prosper na Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Benedicto  Baragomwa

 

Benki ya NMB imekabidhi msaada wa mabati 565 yenye thamani ya Shilingo. Milioni 17 kwa shule tatu za msingi
Wilayani Kisarawe mkoani Pwani, uliopokelewa na Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo, aliyeukabidhi kwa Mkuu wa
Wilaya (DC) hiyo, Jokate Mwegelo.

 

Hafla ya kukabidhi msaaada huo ilifanyika leo, katika Shule ya Msingi Chanzige, mjini Kisarawe, huku shule
zilizonufaika na msaada huo zikiwa ni Shule ya Msingi Kurui Chole (mabati 200), Msegamo (mabati 165) na
Kidugalo (mabati 200) zilizoko Maneromango wilayani humo yote yakiwa na tahamani ya Sh. Milioni 17, ambazo ni
sehemu ya asilimia moja ya faida yao kwa mwaka.

Akizungumza wakati akipokea mabati hayo, Waziri Jafo aliipongeza Benki ya NMB kwa namna inavyoacha alama
kwa jamii, kutokana na misaada inayotoa katika vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya na Mikoa mbalimbali hapa nchini kupitia
Programu ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

Aliitaka NMB kuendelea kusapoti maendeleo ya wilaya ya Kisarawe kama ilivyofanya kwa kutoa elimu na mikopo
ya fedha kwa vikundi mbalimbali, pamoja na Tamasha la Mama Lishe Festival 2020, lililofanyika hapo mapema
mwaka huu.
Naye Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Benedict Baragomwa, aliishukuru Serikali ya Wilaya ya Kisarawe kwa
kuitazama Benki yake kama mdau muhimu wa Elimu na Afya, na kwamba wamejitoa kila wapatapo maombi, ili
kuunga mkono juhudi za Serikali.

‘‘Msaada huu ni sehemu ya utaratibu wetu wa kurejesha kwa jamii asilimia moja ya faida yetu kwa mwaka,
ambapo mwaka huu tuilitenga Sh. Bilioni 1, ambayo inaendelea kutatua changamoto katika Sekta za Elimu, Afya na
Majanga,’’ Baragomwa alisema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate, alimpongeza Waziri Jafo, ambaye ni Mbunge wa Kisarawe
aliyemaliza muda wake na sasa akiwania tena, kwa namna anavyojitoa katika kuleta maendeleo wilayani mwake,
na kwamba wananchi wanapaswa kujivunia uwepo wake.

‘‘Maboresho na mafanikio mbalimbali iliyonayo Kisarawe sasa, siri yake ni uongozi imara wa watu kama Waziri
Jafo, ambaye ameipa mvuto kwa wadau kiasi cha kuzishawishi taasisi kama Benki ya NMB kujitoa kusaidia
masuala mbalimbali ya kijamii hapa Kisarawe,’’ alisema Jokate.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Katibu Tawala Kisarawe, Mwanana Msumi, Ofisa Elimu ya Msingi, Shomari
Bane, huku NMB ikiwakilishwa na Meneja wa Kanda ya Mashariki, Dismas Prosper, na Meneja wa Tawi la Kisarawe,
Justina

Leave A Reply