The House of Favourite Newspapers

Benzema Hatiati Kuwakosa PSG

0

STAA wa Real Madrid, Karim Benzema huenda akaukosa mchezo Robo Fainali wa Copa del Rey na ule wa Hatua ya 16 Bora wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSG, baada ya kuumia wikiendi hii wakati wakicheza dhidi ya Elche.


Benzema aliumia
katika mchezo huo ambao ulimazilika kwa sare ya 2-2 na nafasi yake ikachukuliwa na Luka Jovic.


Imeelezwa kuwa
Benzema anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya Ultrasound kesho Jumanne kujua tatizo lake lina
ukubwa kiasi gani.
Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo atakuwa nje kwa siku 8 mpaka 10 na kwa maana hiyo
mchezo dhidi ya Bilbao
wa Copa del Rey anaweza kukosekana au ule dhidi ya PSG.


Kwa maana hiyo,
Madrid katika mchezo huo wa Copa del Rey itamkosa Benzema, Eder Militao, Vinicus Junior, Rodrygo Goes na Casemiro hawa watakuwa timu ya Taifa ya Brazil na watamkosa pia Federico Valverde (Uruguay) na nahodha wao Marcelo.

KWA KUJIAMINI, AMBUNDO ALIYEWAUA POLISI TZ, AWAAMBIA MASHABIKI – “TULIENI UBINGWA TUNACHUKUA”

Leave A Reply