The House of Favourite Newspapers

BETHIDEI YA JIKE SHUPA… ‘CHURA ’ WAFANYA SHOO YA LAANA

DUNIA ina mambo! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya wikiendi iliyopita wanawake wenye ‘chura’ kufanya shoo ya laana na kuwaacha watu midomo wazi wakiwemo watoto wadogo.

Tukio hilo la aina yake lilitokea wikiendi iliyopita kwenye bethidei ya muuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ iliyofanyika nyumbani kwake Mwananyamala, Dar ambapo kibao kata kilikuwa kinafanya kazi yake na kusababisha wanawake kukata mauno na kuruka sarakasi za aina yake kwa stairi ya kichura chura iliyopelekea wanaume kuwaita Chura.

Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na watu kibao akiwemo msanii wa filamu na mtangazaji, Benny Kinyaiya na Mwanamuziki Sholo Mwamba ambapo kulikuwa na vituko kibao ikiwemo wanaume wakware kubaki midomo wazi na kutoa udenda wakati wanawake hao wakitikisa ‘chura’ wao.

Kibao kata kilipokuwa kikiendelea wanawake waliokuwa wamevalia sare za madera walionesha shoo ya laana kwani walikuwa wanalala chini na kuonyesha umahiri wao wa kusokota nyonga.

Ilifika wakati mmoja wa wanawake hao alimvamia mpiga ngoma wa kibao kata na kumkalia miguuni na kuanza kumtikisia chura hali iliyosababisha wahudhuriaji kulipuka kwa shangwe la aina yake.

Wakati huo Jike Shupa alikuwa na kazi ya kuwazungukia wanawake hao waliokuwa wanasokota nyonga na kuwashushia nguo zao ili maungo nyeti yasionekane kwani kwa walivyoonekana walikuwa hata hawajavaa ‘kufuli’.

“Ohh jamani! uswahilini kuna vituko sana, hii si ni laana maana angalia hawa wanawake wanavyokata mauno na kukatisha vyura wao ukizingatia hapa kuwa watoto wadogo sijui wanajifunza nini.

“Shoo kama hizi zinatakiwa zifanyike ukumbini ambako watoto hawaruhusiwi kuingia lakini kwa hapa ilipofanyika siyo mahali pake kwa sababu watoto wote wako hapa wameacha kwenda kulala majumbani mwao wamekuja kuangalia laana hizi, serikali ingeangalia na hili la shoo za uswahilini jamani,” alisema mama Ester ambaye alikuwa akishuhudia shoo hiyo.

Tofauti na shoo hiyo ya laana kutokana na walivyokuwa wanacheza, waalikwa walikula na kunywa kwani Jike Shupa alijiandaa vyema.

STORI: Gladness Mallya, Risasi Mchanganyiko

Comments are closed.