The House of Favourite Newspapers

WANYAMA 10 WENYE AKILI ZAIDI DUNIANI

1. Sokwe
Sokwe ni viumbe wa pili kwa kuwa na akili zaidi baada ya binadamu.  Kwa mujibu wa uchunguzi wa kisayansi, binadamu alitoka katia familia ya sokwe ambao ni pamoja na nyani, kima, tumbili, na kadhalika.
Sokwe wana uwezo mkubwa wa kuwasiliana, kufahamu mazingira waliyomo, kujenga makazi yao na kutumia zana katika kutafuta chakula chao, wanaweza kujifunza maneno na lugha ya binadamu na hujilinda kwa kutumia zana mbalimbali.
2. Pomboo
Pomboo ndiyo  wanafuatia.  Ni wanyama ambao binadamu huwatumia kutatua matatizo mengi  hususan ya baharini.    Akili ya pomboo ni kubwa kama miili yao, huonyesha hisia mbalimbali, hujifunza vyema mazingira yao, nusu tu ya akili yake huala, nusu nyingine ikiwa macho kukabiliana na tishio lolote.
3. Tembo
Tembo wana akili kubwa kuliko mnyama yeyote wa ardhi kavu.  Huonyesha akili nyingi kijamii na ni moja ya marafiki wakubwa wa binadamu.  Hujfiunza mazingira yao, hutambua milio mbalimbali, huonyesha furaha, hucheza na kusikitika. Huigiza pia sauti mbalimbali na hutafuta chakula kwa kutumia zana.
4. Nyangumi
Wana uwezo mkubwa wa kutumia akili zao katika kuwasiliana na kuigiza sauti mbalimbali, mambo yanayowafanya kuwa wanyama wenye akili zaidi.  Ni watulivu, wanapenda kusafiri na kuwinda.
5. Mbwa
Ni marafiki wakubwa wa binadamu, ambapo mbwa wa kawaida ana akili kama mtoto wa binadamu mwenye umri wa miaka miwili.  Wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu, kujilinda, na kujifunza kutoka kwa binadamu.6. Pweza
Pweza ni viumbe wenye akili zaidi miongoni mwa wale wasio na auti wa mgongo.  Wana uwezo mkubwa wa kujua maadui, mnyama pekee wa kundi hilo kutumia zana, hujibadili kukwepa maadui.

7. Nguruwe

Mmoja wa wanyama wenye akili nyingi, hupenda kucheza na kushirikiana na viumbe wengine, wana uwezo mkubwa wa utambuzi kuliko mbwa, huenda kuishi pamoja, ana uwezo wa kurejea nyumbani hata akiwa mbali, hutambua sauti za viumbe wengine kiurahisi.

8. Fisimaji

Ni wanyama wadogo zaidi wa majini wanaoishi majini na nchi kavu, hutumia mawe kutafutia chakula na kuondoa sehemu za samaki na kaa wakati wa kuwala, wana uwezo wa kutambua sauti za adui.
9. Kunguru
Hawa wamezagaa duniani kote, hawawapendi binadamu na huwafanyia fujo wanapoweza, wana akili kubwa ya kutafutia chakula, miongoni mwa ndege wenye akili zaidi, wanatambua kirahisi mavi ya binadamu, wanaweza kuvunja nazi kwa kuiangusha kwenye mawe, hutumia mawe kushambulia maadui na kushambulia ndege wengine.
10. Mchwa
Hawa hawana akili kubwa, wamekuwepo tangu enzi za wanyama ‘dinosaur’ walipokuwa wanaishi, wana akili ndogo zaidi miongoni mwa viumbe mbalimbali.  Walianzisha mfumo wa kilimo miaka milioni 50 kabla ya binadamu kwa kupandikiza na kukusanya chakula.  Mchwa anaweza kubeba kitu kikubwa mara 50 zaidi ya mwili wake kutokana na misuli ya nguvu aliyo nayo.

Comments are closed.