The House of Favourite Newspapers

DENTI MORO ABAKWA, ASHONWA NYUZI 7

MOROGORO: Binti wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Kisanga (jina linahifadhiwa) mkazi wa Msolwa, Kata ya Kisanga, Mikumi amefanyiwa ukatili wa kubakwa na kulawitiwa na kijana aliyefahamika kwa jina moja la Alphan.

 

Akizungumza na Uwazi, mjomba wa mwanafunzi huyo, Salum Makinda alisimulia hivi: “Ilikuwa June 14, mwaka huu mpwa wangu alirudi nyumbani akiwa hoi lakini wazazi wake hawakuwepo walikuwa wamesafiri, nikapigiwa simu na kufika pale nikawaita ndugu zangu wengine wa familia na kumuuliza nini kimemkuta.

“Alidai kuwa wakati anatoka kuchukua deli la maandazi dukani, njiani alikutana na Alphan, akamkamata ghafla yeye akajitoa mikononi mwake na kufanikiwa kukimbia lakini mtuhumiwa alimkimbiza na kumkamata.

 

“Alisema kijana huyo alimtolea kisu na kumwambia akipiga kelele atamuua baada ya hapo akamuingiza kichakani, akamchania nguo za ndani na kuanza kumfanyia unyama huo wa kumbaka na kumlawiti.

“Baada ya hapo tukaenda kituo cha polisi na kupata PF3 kisha tukampeleka katika kituo cha afya Msange ambapo alipata huduma ya kwanza na baadaye tukampeleka Hospitali ya St. Kizito, Mikumi na akashonwa nyuzi saba kwenye makalio kwa kuwa aliharibiwa sana,” alidai mjomba huyo.

 

Baada ya hapo mjomba huyo alisema kuwa Mkuu wa Kituo cha Polisi Kata ya Kisanga alifika eneo la tukio na kuchukua nguo iliyochanwa pamoja na mtuhumiwa na kupelekwa kituoni.

“Mke wa mtuhumiwa alikwenda kituoni hapo na kutaka wazungumze ili yaishe lakini mkuu wa kituo aligoma na kumpeleka katika Kituo cha Wilaya cha Ruhembe ambapo alilala, hata hivyo, alipewa dhamana,” alidai mjomba.

 

Uwazi lilimtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Ulrich Matei hakupatikana hewani lakini afisa mmoja wa polisi mkoani Morogoro ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini kwa kuwa siyo msemaji alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kesi hiyo ilifunguliwa polisi kwa jalada namba KSN/RB/32/2018 na KSN/ IR/14/2018.

STORI: NEEMA ADRIAN, UWAZI

Comments are closed.