‘BETIKA’ LAWAPAGAWISHA WAZEE WA KUBETI TABATA DAR

NI wiki ya tano sasa imetimia tangu Gazeti la Betika liingie mtaani ambapo safari hii wazee wa kubeti katika mitaa mbalimbali ya Tabata jijini Dar es Salaam, wameonesha furaha yao juu ya gazeti hilo linalotolewa bure. 

 

Betika linalogawiwa bure kwa watu kuanzia umri wa miaka 18 na kutoka mtaani kila Jumatano, limezidi kuwapagawisha wengi hasa wazee wa kubeti kutokana na gazeti hilo kuhusika na ishu nzima za kubeti.

 

Katika kuzidi kulitangaza gazei hilo, timu ya maofisa masoko wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inachapisha gazeti hilo, leo Jumatano iliingia mitaa ya Tabata-Bima, Kimanga, Kisukuru na Chang’ombe, na kukutana na wasomaji ambao walilipongeza.

Mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo aliyejitambulisha kwa jina la Masoud, alisema: “Kwa kweli hili gazeti nimekuwa nikilifuatilia tangu lilipoanza kutokNAa na limekuwa msaada mkubwa kwangu katika masuala ya haya kubeti.  Tangu lianze kutoka nimekuwa nikilisoma na kuona wenzangu wakipiga nalo picha, sasa leo mmenifikia, hivyo naomba na mimi nipige nalo picha ili furaha yangu itimie.”

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema, alizidi kukazia kwamba wamekuwa wakipokea maoni na kuyafanyia kazi juu ya kuliboresha gazeti hilo ili kuwapatia wasomaji vile vitu wanavyotaka kuvisoma.

“Kila linapokuwa mtaani gazeti hili, tunakutana na wasomaji na kuwaomba kutoa maoni yao ya nini kifanyike kwa ajili ya kuliboresha. Kikubwa ni kwamba kila siku tumekuwa tukiliboresha kwa sababu lile toleo la kwanza na hili utaona kuna marekebisho makubwa sana.

“Mbali na maboresho hayo, pia tunawaalika watu mbalimbali kuja kutangaza nasi kwani nafasi za kufanya hivyo zipo wazi, wasisite kuja ofisini kwetu Sinza-Mori jijini Dar kwa ajili ya kuleta matangazo yao hayo,” alisema Mgema.

Gazeti hilo lenye kurasa 20 ambazo zote ni za rangi, mbali na kuwa na makala na ‘odds’ za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya.

Matukio katika Picha:

 

 

MWANDISHI WETU


Loading...

Toa comment