The House of Favourite Newspapers

Kadinali aliyelawiti watoto ahukumiwa kwenda Jela

 

JJI Mkuu wa mahakama moja nchini Australia, Peter Kidd, amemhukumu kifungo cha miaka sita gerezani Kardinali George Pell baada ya kukutwa na hatia ya kuwalawiti wavulana wawili.

 

Shirika la habari la ABNA limeripoti kuwa kadinali huyo aliwalawiti  wavulana wawili waliokuwa wakiimba kwaya katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patrick, Melbourne, zaidi ya miaka 20 iliyopita.

 

Jaji Kidd ameamuru leo kuwa Pell atumikie kifungo cha miaka mitatu na miezi minane gerezani kabla ya kustahili kupatiwa msamaha.

 

Pell aliyekuwa waziri wa uchumi wa Vatican, alikutwa na hatia mwezi Desemba mwaka uliopita kwa kumlawiti mvulana wa miaka 13 na kumdhalilisha kinyume cha maadili mvulana mwingine pia mwenye umri wa miaka 13 mwishoni mwa miaka ya 1990.

 

Visa hivyo vilitokea miezi michache baada ya Pell kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Melbourne. Pell mwenye umri wa miaka 77 amekana mashtaka dhidi yake na mwezi Juni atakata rufaa kuipinga hukumu hiyo.

 

Hata hivyo wananchi wengi wamelaumu hukumu hiyo na kudai kuwa alitakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka mingi zaidi.        Mashtaka ya viongozi wa Kanisa Katoliki ya kubaka na kulawiti watoto, yamekuwa mengi sana, na bado mpaka sasa hayajatolewa hukumu.

Comments are closed.