The House of Favourite Newspapers

Betika lipo mtaani leo

NI takriban mwezi mmoja tangu lilipoingia mtaani, Gazeti la Betika, Jumamosi iliyopita lilikuwepo Uwanja wa Taifa ambapo Simba iliweka historia ya kushinda mchezo na kuingia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Simba ilishinda mabao 2-1 dhidi ya AS Vita Club ya DR Congo na kushika nafasi ya pili katika Kundi D, lakini kuelekea mchezo huo mitaa ya Temeke kwenye Uwanja wa Taifa, kulikuwa na idadi kubwa ya mashabiki wa Simba na wa timu nyingine mbalimbali ambao waliburudika kwa kupata nakala zao za Betika bure.

 

Gazeti hilo la bure ambalo linakuwa na takwimu mbalimbali, habari, makala, uchambuzi na matangazo, lilikuwa lulu kwa maelfu ya mashabiki waliojitokea uwanjani hapo hasa kabla ya mchezo kuanza.

Betika linalogawiwa bure kwa watu kuanzia umri wa miaka 18 na kutoka mtaani kila Jumatano, lilishikwa mikononi na wanasoka wengi ambao walionyesha wazi kuvutiwa nalo ndani ya uwanja na nje.

 

Akizungumza kuhusu usambazaji wa Gazeti la Betika, Ofisa Masoko wa Global Publishers, Mussa Mgema alisema: “Kila linapokuwa mtaani gazeti hili, tunakutana na wasomaji na kuwaomba kutoa maoni yao ya nini kifanyike kwa ajili ya kuliboresha, kikubwa ni kwamba kila siku tumekuwa tukiliboresha kwa sababu lile toleo la kwanza na hili utaona kuna marekebisho makubwa sana.

 

“Kwa wale wanaohitaji kutangaza kupitia gazeti letu la Betika kwa mawasiliano zaidi wafike ofisini kwetu Sinza Mori kwenye jengo la Global Group jijini Dar es Salaam, au wawasiliane nasi kwa namba, 0755-826488, 0712-595636 na 0659-472001 au barua pepe, betika255@gmail. com.”

Comments are closed.