The House of Favourite Newspapers

Betika ndiyo habari ya mjini

 

WASOMAJI wa Gazeti la Betika, wameendelea kutoa ushuhuda wao juu ya gazeti hilo huku wakisema ni habari ya mjini kwa sasa katika masuala yote ya kubeti.

 

Gazeti hilo lenye kurasa 20 za rangi, hutolewa bure kwa watu wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea ambalo huchapishwa na Kampuni ya Global Publishers.

 

Betika mbali na kuwa na makala na odds za kampuni mbalimbali, pia kuna takwimu za ligi kubwa barani Ulaya ambazo wasomaji wengi wanalitumia kutandaza mikeka yao.

 

Kila Jumatano ambapo Betika huingia mtaani, timu ya maofisa masoko wa Global Publishers hutembelea mitaa mbalimbali ambapo leo Jumatano ilikuwa maeneo ya Kawe, Masaki, Msasani na Kariakoo, ikakutana na wasomaji kadhaa waliotoa maoni yao.

 

 

“Betika limekuwa habari ya mjini kwa sasa kwani linatusaidia sana sisi wazee wa kubeti. Hapo kabla ya uwepo wa gazeti hili, tulikuwa tunabeti lakini hatushindi kirahisi kama sasa.

 

 

“Uzuri wa gazeti hili linakurahisishia kazi ya kubeti, ukiangalia ndani kuna ukurasa mzima unaozungumzia mechi ambazo unaweza kubeti, lakini zile takwimu zake zinasaidia wakati wa kubeti kufahamu timu gani ina ubora kiasi gani.

 

 

“Kutokana na hilo, ni wazi Betika litaendelea kuwa juu na niwaombe wanaoliandaa, waendelee kuwa wabunifu zaidi kwa lengo la kutusaidia sisi tunaobeti tuweze kuendelea kushinda mara kwa mara,” alisema mmoja wa wasomaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamza akiwa maeneo ya Kawe.

 

 

Ndani ya Betika, bado kuna nafasi za kutangaza ambapo kwa yeyote anayehitaji kutangaza na gazeti hilo anakaribishwa ofisini Sinza Mori jijini Dar.

Comments are closed.