The House of Favourite Newspapers

Bi. Chau Aanika siri ya kuonekana kijana miaka yote!

0

BI CHAU (6)Chausiku Salumu ‘Bi. Chau’.

MAMBO vipi mpenzi msomaji wa safu yetu ya Mpaka Home, kama ilivyo kawaida mpenzi msomaji wangu najua unapenda kujua maisha halisi ya mastaa wetu mbalimbali Bongo, basi leo tunaye mkongwe wa enzi na enzi katika tasnia ya uigizaji huyu si mwingine ni Chausiku Salumu ‘Bi. Chau’.

Msanii huyu anaishi Magomeni-Kagera jijini Dar, ambapo anaishi yeye, dada wa kazi na mjukuu wake. Mume wake ambaye hajamtaja jina amesema ni mtu wa kusafiri, si mkaaji sana nyumbani hapo.

Ungana nami katika mahojiano niliyofanya naye:

BI CHAU (1)Nini anachopenda kukukifanya kila siku anayokuwa nyumbani?

Mimi bila kufanya usafi wa nguvu nyumbani kwangu bado sijasikia raha kabisa ni lazima niamke asubuhi na mapema kama mawanamke anavyotakiwa kisha nafanya usafi nyumba yangu yote na hata mazingira ya nje baada ya hapo najifanyia usafi wangu wa mwili.

BI CHAU (4)Shughuli gani nyingine zinazomfanya awe bize?

Mimi kama unavyojua ni mtangazaji pale Radio One pia mbali hilo nafanya shughuli za ukungwi hivyo napanga muda wangu kuhakikisha shughuli zote hizo nazifanya kwa pamoja.

BI CHAU (3)Mapishi ya nyumbani anaingia mwenyewe jikoni?

Kwa kweli chakula cha baba yenu lazima nipike kwa mkono wangu mwenyewe na ninaona faraja sana kupika chakula kuliko kitu chochote, marufuku dada wa kazi tena sasa hivi ndiyo nimeweka dada kwa ajili ya kazi lakini zamani nilikuwa naimiliki nyumba mwenyewe kama mwanamke.

BI CHAU (5)Naona una ‘kitochi’, hautaki kumiliki simu za kisasa?

Sitaki kabisa simu za kisasa zitanipotezea muda wangu wa kazi na hata kufanya kazi za kumuandalia baba maana haya mambo ya ‘WhatsApp’ mara ‘Facebook’ yanaharibu sana ndoa na kwa nini niharibu nyumba yangu kwa vitu ambavyo havikuwepo tangu enzi na enzi.

BI CHAU (7)Anashirikiana na majirani zake?

Kwa kweli maisha ninayoishi na majirani zangu ni mazuri sana na sina tatizo na mtu na hivi sasa nimewaunganisha kwani tuanzisha kikundi chetu kinaitwa Maendeleo cha akina mama, kuliko kubweteka bora kutafuta njia ya kujikwamua.

BI CHAU (8)Nini siri ya kuonekana msichana kila wakati?

Ni kujipenda tu maana kama mimi unavyoniona siwezi kutoka ndani bila kujifukiza udi na hata nguo yangu ninayovaa lazima inukie udi kwa hiyo kujipenda ndiyo silaha kubwa maana mtu anapojiweka ‘rafu’ ndivyo anavyozidi kujizeesha.

BI CHAU (9)Kwa nini mumewe haonekani mara kwa mara?

Yupo baba ila tu anakuwa kazini na mara nyingi anasafiri ila siku nyingine ukija utakumkuta wala usijali kabisa.

KUNUNUA NA KUSOMA MAGAZETI YA GLOBAL PUBLISHERS ONLINE, INGIA HAPA==>VODACOM M-PAPER APP

*********

JIUNGE NA SOCIAL MEDIA ZETU

KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA

INSTAGRAM: @Globalpublishers

ERIC SHIGONGO INSTAGRAM: @ericshigongo

TWITTER: @GlobalHabari

FACEBOOK: @GlobalPublishers

SUBSCRIBE YOU TUBE: Global TV Online

GLOBAL TV ONLINE: www.globaltvtz.com

HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, ERIC SHIGONGO FACEBOOK PAGE:@shigongotz

Leave A Reply