The House of Favourite Newspapers

Bi Leticia: Wanaume Wataalam Wa Kunena Kwa Lugha

0

 

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa,mapema leo amehudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI Dunia,yaliofanyika katika ukumbi wa Ruandazonvwe,Mkoani Mbeya,na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali serekali.

 

Katika maadhimisho hayo ambayo kauli mbiu ni Zingatia usawa,tokomeza UKIMWI,tokomeza magonjwa ya mlipuko,mkurugenzi wa baraza wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (NACOPHA) @nacophatz Bi Leticia Mourice,alilisitiza kuwa wanaume waache kuumiza mioyo ya wanawake,maana mara nyingi wao ndio wanakuwa wanawapa ushawishi mkubwa wanawake na baada ya kuwapa maambukizi wanawaacha na kuwanyanyapa kama sio wao waliowarubuni na kuingia kwenye ngono zembe.

 

” Mimi nachojua wanaume wanaweza kunena mpaka kwa lugha wanapotaka kumrubuni binti lakini akishampata basi anamdiliti na huku tayari kamuachia maambukizi na kiumbe tumboni ambacho kiko katika hatari ya kupata maambukizi,jamani tutumie silabi tatu tu wanawake,Sitaki,hapana,bado” alisema Bi Leticia.

 

Pia mkurugenzi huyo aliongeza kuwa,siku hizi hakuna wanaoishi na matumaini bali wanaoishi na malengo,kwa maana hata katika baraza lake zipo familia ambazo mmoja anaishi na maambukizi na mwenza wake hana,lakini hakuna unyanyapaa na hata kwa upande wake yupo na mumewe ambao tayari wana maambukizi na hakuna unyanyapaa hata kidogo.

 

Viongozi waliohudhuria maadhimisho hayo walitoa pongezi kubwa kwa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) @tacaidsinfo kwa kuweza kupambana na kupiga vita maambukizi hayo ili kufikia 95 ya 95 kwa malengo yaliyoweka.

 

Katika maadhimisho hayo pia kulikuwa na burudani mbalimbali zilitumbuiza akiwepo msanii wa Bongo Fleva,Rayvanny,ambaye alipata nafasi ya kushikwa mkono na waziri mkuu.

Habari @imeldamtema

Leave A Reply