The House of Favourite Newspapers

Bi Samia Awataka Wanafunzi ‘Wakamue’ Sayansi Kufanikisha Sera ya Viwanda

0

MAKAMU  wa Rais wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania, Bi. Samia Suluhu (pichani kushoto) amewataka wanafunzi nchini kujibidiisha katika kusoma masomo ya Sayansi ili kulisaidia Taifa linapoelekea sasa kwenye sera ya Tanzania  ya Viwanda.

Pia, amesema taifa kutokuwa na wataalamu wa sayansi litachangia kurudisha azma ya serikali kufikia malengo ya kuwa na waatalamu wa kuviendesha viwanda hivyo.

Makamu  wa Rais, ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya wanafunzi wanaosomeshwa na taasisi isiyo ya kiserikali inayotetea maendeleo kwa wanawake (WAMA) inayoongozwa na mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete.

Amesema kwa sasa licha ya serikali kujenga maabara takribani shule zote za serikali pamoja na kuajiri walimu wengi wa  sayansi kwenye shule za serikali, ni wajibu wa wanafunzi kusomea masomo ya sayansi.

Mama Salma Kikwete wakati wa mahafali hayo.

Pia, amewaomba wanafunzi hao wa kidato cha sita kutumia fursa ya ukuaji wa mitandao kwa kupata maarifa badala ya kutumia  mitandao hiyo kwenye mambo yasiyofaa katika jamii ambayo amedai yatafifisha juhudi zao za kifikisha malengo yao waliyojiwekea.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete amesema taasisi hiyo itaendelea kuwasomesha wanafunzi wenye mazingira magumu ili wafikie malengo ya kulisaidia taifa.

NA HILLALY DAUDI | GLOBAL TV ONLINE

Hii Ndiyo Hekima ya Mama Salma Kikwete 

Leave A Reply