Biashara, Mwadui FC wamgombea straika Azam FC

KLABU za Biashara United na Mwadui FC, zipo katika vita ya kumuwania mshambuliaji Waziri Junior ambaye ni mchezaji huru baada ya kuachwa na klabu yake ya Azam FC.

 

Mtu wa karibu na mshambuliaji huyo ameliambia Championi Ijumaa, kuwa klabu hizo mbili zimeanza mazungumzo na mshambuliaji huyo ambapo anaweza kutimkia kokote kutokana na kuwa huru.

 

“Kweli klabu hizo zimeanza kuulizia huduma ya Waziri hasa baada ya kuachwa na Azam FC. Klabu ambayo itatoa kiasi kile ambacho mwenyewe anakitaka ndiyo ambayo itaipata saini yake, japo hatujajua ni wapi anaweza kwenda,” alisema mtu huyo.

 

TFF Yashindwa ‘KUJIZUIA’ Yawajibu Wanaomsema Kocha AMUNIKE “Mnawakatisha Tamaa”

Loading...

Toa comment