The House of Favourite Newspapers

BIASHARA TAMU KINOMA KWA WEMA!

Wema Isaac Sepetu.

 

ASIKWAMBIE mtu! Staa mwenye nyota kama zote Bongo, Wema Isaac Sepetu amefunguka kuwa hakuna kitu anachokipenda kama biashara anayoifanya hivi sasa ya kuuza nguo za watoto kwani imekuwa tamu kinoma.

 

Akizungumza na Ijumaa, Wema alisema anaanza kuona utamu wa biashara hiyo ndiyo maana sasa hivi hapati usingizi kama zamani.

“Biashara ni tamu kinoma ukiweza kuipatia. Kufanya biashara ambayo unaipenda ni jambo la msingi sana. Nafurahia kazi yangu hii, kuna vitu nimejifunza pia,” alisema Wema ambaye anamiliki duka hilo la nguo alilolipa jina la Little Sweetheart lililopo Mwananyamala, Koma-Koma jijini Dar.

STORI NA IMELDA MTEMA | GPL

Comments are closed.