The House of Favourite Newspapers

Mpenzi Wa Poshy Anapata Tabu Sana!

Jacqueline obed ‘Poshy Queen’

 

ANAPATA tabu sana! Mrembo anayetingisha kwenye mitandao ya kijamii (socialite) kutokana na figa yake matata, Jacqueline obed ‘Poshy Queen’ amefunguka kuwa anamuonea huruma mpenzi wake kwa vile anapata tabu sana kutokana na umbo lake.

 

Akizungumza na Ijumaa, Poshy alisema kutokana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanaume wenye uchu wanaotaka kuwa na uhusiano naye kimapenzi, mpenzi wake huwa anapitia kipindi kigumu.

“Kuna wakati namuonea huruma kutokana na usumbufu ninaoupata hivyo huwa anajitahidi kupambana na hali hiyo. Kuna wakati unamuona kabisa amekata tamaa, lakini nampa moyo kila siku,” alisema Poshy.

Comments are closed.