The House of Favourite Newspapers

Biashara United Mara Yaingizwa Sokoni

0

Klabu ya soka ya Biashara United ya mkoani Mara iliyokuwa ikimilikiwa na wanachama, kwa sasa imepata mmiliki mpya ambaye ni Free Sports LTD ambao wataimiliki klabu hiyo kuanzia msimi wa mwaka 2023/2024 ambapo kampuni hiyo itasimamia shughuli zote za uendeshaji wa klabu hiyo kuhakikisha inapanda daraja kucheza ligi kuu Tanzania bara kwa mara Nyingine.

Akizungumza na Global Publishers Katibu mkuu wa Biashara United Mariam Lima amesema “Ni kweli timu yetu imebadilishwa jina kutoka Biashara United mara kuwa Mara United Football Club na lengo la kubadilisha jina ni kuhakikisha kwamba timu hii inahudumiwa ipasavyo tofauti na hali ilivyo kwa sasa na mpango ni kuona timu yetu ikipanda daraja kucheza ligi kuu kwa msimu wa mwaka 2023/2024”

Zoezi la kukabidhiwa kwa nyaraka za usajili pamoja na Katiba ya Klabu hiyo lilifanyika february 27 mwaka huu mkoani Mara ambapo mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali Seleman Mzee ndiye aliyekabidhi nyaraka hizo huku lengo kuu ikiwa ni kuhakikisha timu hiyo inajiendesha bila vikwazo ili iweze kupanda daraja na wakazi wa Mkoa huo waweze kupata burudani ya soka.

Biashara United ilishuka daraja msimu wa mwaka 2021/2022 ambapo kwa msimu wa mwaka 2022/2023 imekuwa ikicheza mashindano ya Championship ambapo kwa sasa iko nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi hiyo baada ya michezo 18 ambapo timu hiyo imefanikiwa kujikusanyia jumla ya alama 19 ambapo inapigana kuhakikisha inabaki ligi hiyo kutokana na ushindani katika ligi hiyo kuwa mkubwa.

 

Leave A Reply