The House of Favourite Newspapers

Bibi wa Miaka 65 Auawa kwa Kung’atwa na Mbwa Watano

0
Aina ya Mbwa aliyetajwa kumng’ata Bibi

BIBI mwenye umri wa miaka 65, Ann Dunn ambaye ni raia wa Marekani ameshambuliwa na mbwa watano ambao walimng’ata na alipopekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu taarifa zilitoka kuwa amefariki dunia.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Daily Mail, Dunn aliuawa na mbwa hao aina ya bulldogs akiwa ndani ya nyumba yake iliyopo St. Brigid’s Crescent huko Vauxhall Liverpool.

 

Polisi wakiwa wameimarisha usalama eneo la tukio

Kabla ya Ann kung’atwa na mbwa alitakiwa kwenda  shuleni kumchukua mjukuu wake na siku hiyo hakufika shuleni ndipo ndugu wakafuatilia na kugundua kuwa amepatwa na kitu kibaya.

 

Polisi wa Merseyside nchini Marekani wamesema kuwa bibi huyo aling’atwa na mbwa mwaka jana katika eneo la kuzaliana mbwa huko Liverpool ikiwa ni baada ya kudhulumiwa mbwa wawili.

 

Polisi wa Merseyside wamesema bibi Ann alikutwa akiwa ameanguka chini nyumbani kwake na kwamba uchunguzi wa mwili wake utafanywa ili kubaini chanzohalisi cha kifo chake.

Usalama eneo la tukio

Hayo yamejiri baada ya Dunn kuhitaji matibabu hospitalini mnamo Agosti, 2021 kitokana na kungatwa mara kadhaa na mbwa waliosababisha majeraha katika mwili wake.

 

Mwanaume mwenye umri wa miaka 31 alikamatwa na Polisi kwa tuhuma za kumiliki mbwa kwa njia hatari bila kudhibitiwa lakini tayari amepewa dhamana kwa sharti la kusubiri uchunguzi zaidi.

 

Imeandaliwa na Sanifa Khalifa kwa msaada wa mtandao

Leave A Reply