The House of Favourite Newspapers

Utafiti wa Kisayansi Wabaini Kuongezeka kwa Usugu wa ARV kwa Wajawazito

0

 

MKURUGENZI wa Takwimu, Mifumo, Utafiti na Ufatiliaji wa Taasisi ya Management and Devolopment for Health (MDH) Lameck Machumi, ameweka wazi ripoti ya utafiti uliofanywa na taasisi hiyo kuhusiana na na usugu wa matumizi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi (ARVs) kwa akina mama wajawazito.

 

Katika ripoti ya utafiti huo, Machumi amebainisha kwamba kumekuwa na matumizi ya dawa ambazo nyingi zimeshakuwa sugu kwa watumiaji na kusababisha ongezeko la maambuki kwa mama wajawazito kwenda kwa watoto kwa asilimia 27.5, tofauti na miaka ya nyuma.

 

Mkurugenzi huyo ameyasema hayo kwenye sehemu ya maandalizi ya kongamano la kila mwaka la afya la Tanzania Health Summit litakalowaleta pamoja serikali, sekta binafsi na wafanyabiashara, linalotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 11 hadi 13, 2022 jijini Dar es Salaam.

 

Amesema kuwa Wizara ya Afya, inapaswa kuangalia upya jinsi ya kuleta dawa nyingine ambazo zitaendelea kupunguza makali ya virusi hivyo, ili ziweze kuondoa usugu kwa watumiaji.

 

Kongamano hilo linalotarajia kufanyika ni la 9, tangu lilipoanzishwa mwaka 2014.

Leave A Reply