The House of Favourite Newspapers

Bidhaa za Red Gold Zatajwa Kuwa Na Faida Za Kiafya Kwa Walaji

0

RED Gold ni nembo ya kibiashara ambayo ndani yake kuna bidhaa mbalimbali zikiwemo Tomato Sauce, Chilli Sauce, Jam, Juice, Tomato Ketchup, Pilipili Mbuzi Sauce, Tomato Paste na Pickles na kwa kipindi kirefu sasa bidhaa hizo zimeendelea kuwa chaguo la kwanza kwa watu wengi.

Licha ya ladha nzuri ambazo bidhaa hizo zimekuwa nazo kwa kipindi kirefu, utafiti unaonesha kwamba pia zinatoa faida nyingi za kiafya kwa walaji wake.

 

Miongoni mwa faida za bidhaa za Redgold zinazozalishwa na Darsh Industries Ltd ni kupunguza hatari ya saratani ya matiti, kupunguza kansa ya kibofu hatarishi, kukinga ngozi kupata madhara mbalimbali na kupunguza mafuta yanayoganda kwenye mishipa ya damu.

Sababu nyingine ni kuongeza uwezo wa kuona, kuboresha afya ya mifupa na kuongeza idadi ya mbegu za kiume.

“Kupitia matangazo mbalimbali kwenye vyombo vya habari, nimejifunza kwamba mbali na ladha nzuri ambazo zinapatikana kwenye bidhaa za Red Gold, lakini pia kuna faida nyingi za kiafya.

“Hilo limenifanya niwe natumia bidhaa hizi tu, tofauti na nyingine zinazotengenezwa kienyeji zikiwa na kemikali nyingi,” alikaririwa Aisha Mahmood, mwanadada anayefanya biashara ya vyakula ikiwemo chips Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

“Tangu tuanze kuzalisha bidhaa zetu, tulijikita kuleta tofauti kwa walaji. Tunasimamia uzalishaji wa mbogamboga na matunda yanayotumika kwenye utengenezaji wa bidhaa zetu.

“Tunazingatia sana usafi na ubora wa bidhaa zetu kuanzia mwanzo kabisa na hiyo ndiyo sababu iliyofanya tuzidi kupata wateja wengi ndani na nje ya nchi,” alikaririwa Badrish Pandit, Mkurugenzi Mkuu wa Darsh Industries Ltd.

Naye Joseph Mwananzila, mfanyabiashara wa chipsi eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam, alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na bidhaa za Red Gold:

 

“Kwa miaka mingi nimekuwa nikifanya biashara ya kuuza chipsi na mwanzo wateja walikuwa wakilalamikia tomato sauce na chili sauce nilizokuwa nazitumia lakini tangu nilipoanza kutumia bidhaa za Redgold, wateja wanafurahia kwelikweli na wanazidi kuongezeka kila kukicha, bidhaa hizi ni bora sana.”

 

Kampuni hiyo imekuwepo nchini tangu mwaka 1999 na ubora wa bidhaa zake umesababisha kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali, huku pia kikiunga mkono kauli ya Rais Dk. John Pombe Magufuli ya kuwaajiri wazawa na kuboresha uchumi wa viwanda nchini.

Pia Darsh Industries imekuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono wasanii wazawa ambapo mwaka 2016, iliingia mkataba na msanii mkubwa wa muziki wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ katika kampeni yake iliyopewa jina la Ladha na Mtonyo ambapo watumiaji mbalimbali wa bidhaa hizo, walijinyakulia mamilioni ya fedha zilizotolewa kama zawadi.

 

“Kampuni yetu pia inafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria za nchi ambapo bidhaa zetu zote zimethibitishwa na Shirika la Ubora wa Viwango (TBS), mamlaka ya Chakula, Dawa na Vifaa Tiba (TFDA) pamoja na wasimamizi wa mazingira bora mahali pa kazi, OSHA,” aliongeza Pandit.

 

Kwa mawasiliano, unaweza kuwapata kwa kufika kiwandani kwao, Themi Industrial Area, Arusha plot namba 16 au kwa kupiga simu 0736 500 525. Unaweza pia kuwacheki kwa barua pepe, [email protected] au tembelea website yao kwa kubofya www.redgold.co.tz

Leave A Reply