Bifu la Uwoya na Tessy, Ukweli ni Huu!

BAADA ya mastaa wawili, Irene Uwoya na Tessy Abdul ‘Tessychocolate’ ambao ni mashosti kudaiwa kuwa kwenye bifu kali kisa kuibiana mwanaume, wenyewe wameibuka na kuweka mambo hadharani.

 

Awali habari zilieleza kuwa wawili hao licha ya kwamba walikuwa marafiki wa karibu sana kwa sasa ni paka na panya kwani wana bifu kali na hata salamu hawapeani.

 

Kutokana na tetesi hizo, Amani liliwatafuta warembo hao kila mmoja kwa wakati wake ili kuanika ukweli ambapo lilianza na Tessy ambaye ndiye anadaiwa kumchukua mwanaume wa Uwoya ambaye alikuwa anamuweka mjini.

 

Tessy aliliambia Amani kuwa amezoea sana kusikia maneno ya kizushi ambayo hayana ukweli kama haya ya kuwa na bifu na Uwoya na mara nyingi watu wanayazungumza kwenye mitandao ya kijamii.

 

“Nasikitika sana kila kukicha watu wa kwenye mitandao wanajadili mambo ambayo hayana msingi hata kidogo, mimi na Uwoya ni marafiki sana hatuna tatizo lolote linalotugombanisha, kama hatuonekani pamoja ukweli ni kwamba kila mtu yuko bize kutafuta maisha na si kitu kingine,” alisema Tessy na kuwaomba watu waacha maneno ya ugombanishi.

 

Kwa upande wa Uwoya alisema kuwa hakuna kitu kama hicho na mwanaume anayezungumziwa ni nani hadi afikie hatua ya kuwagombanisha, wako vizuri na hao wanaojisikia kusema waendelee tu hawamuathiri chochote.

 

“Eti mwanaume ametugombanisha! Ni yupi huyo? mambo hayo kwanza hayana nafasi kwetu ila siwalaumu watu hasa wa mitandaoni maana kazi yao ni kulala na kuamka na kuanza kuzua maneno yasiyokuwa na mbele wala nyuma,” alisema Uwoya.

Stori: Imelda Mtema, Amani


Loading...

Toa comment