The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Kenny Rogers Afariki Dunia

0

Los Angeles, Marekani. Nyota wa muziki wa country, Kenny Rogers, ambaye amekuwa katika muziki kwa miaka 60, amefariki akiwa na umri wa miaka 81, familia yake ilisema jana jioni.

 

“Rogers amefariki kwa amani akiwa nyumbani kwake na kifo chake ni cha kawaida. Amefariki akiwa chini ya uangalizi na akiwa amezungukwa na familia yake,” imesema taarifa ya familia.

 

Mwimbaji huyo mzaliwa wa  Texas alijulikana kwa nyimbo zake zilizotamba duniani kama “The Gambler,” “Lucille” na “Islands in the Stream.”

Leave A Reply