The House of Favourite Newspapers

Bilionea MO Afanya Kufuru Usajili Simba Avunja Mkataba wa Staa wa Cameroon

0
Bilionea Mohamed Dewji.

HUKO Simba sasa ni vicheko tu, mara baada ya uongozi wa juu wa timu hiyo kuanza kushusha majembe ya maana huku wakiwa wanapewa nguvu kubwa kutoka kwa Rais wao wa heshima na mwekezaji wa timu hiyo, Bilionea Mohamed Dewji.

Imefichuka kuwa Bilionea MO amefanikisha dili la Mcameroon, Che Fondoh Malone na kulazimika kuvunja mkataba wa staa huyo wa Cotton Sports ya Cameroon kwa dau la dola 100,000 (Zaidi ya Sh 230Mil za Kitanzania).

alitumiwa mkataba na baadhi ya nyaraka kwa ajili ya kuzipitia kabla ya kusaini mkataba huo wa miaka miwili.

Mcameroon, Che Fondoh Malone.

“Kilichobakia kwa Malone ni kukamilisha taratibu za uhamisho katika klabu yake ya Cotton Sports baada ya kufikia makubaliano ya kumuachia ajiunge na Simba katika msimu ujao

“Hiyo baada ya kutokea vuta nikuvute kati ya Simba na Cotton Sports iliyotaka kitita hicho cha fedha ili muachie ambacho Simba walikuwa hawapo tayari kutoa pesa hizo.

“Simba imefanikisha dili hilo haraka na tayari staa huyo ametakiwa kutua nchini haraka kwa ajili ya utambulisho na acheze michuano ya Super Cup,” alisema bosi huyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ juzi alizungumzi hilo la usajili

kwa kuwaambia mashabiki wa timu hiyo, kuwa “Tumepanga kufanya usajili katika kuelekea usajili wa msimu ujao.

STORI: WILBERT Molandi, Dar es Salaam

UMAFIA! SIMBA SC YAMSHUSHA NGOMA DAR/ WINGA MPYA YANGA ATUMIWA TIKETI/ MO ATOA AHADI NZITO..

Leave A Reply