The House of Favourite Newspapers

Bill Nas Apiga Chini Muziki

0

STORI: Boniphace Ngumije | RISASI JUMAMOSI

MSANII wa Bongo Fleva, Bill Nas amefunguka kuwa kwa sasa ameamua kuupiga chini muziki ili kuhakikisha anashiriki vyema na kutumia muda wake wote kwenye masomo aliyobakiza katika Chuo cha Biashara (CBE).

Akichonga na Mikito Nusunusu, Bill Nas alisema kuwa, chuoni hapo anaposomea masomo ya ‘Procurement and Supply’ amebakiza muda wa mwezi mmoja ambapo katika kipindi hicho akiwa bize na masomo ameamua kuweka kando masuala yote yanayohusiana na muziki.

“Shule ni muhimu pia, nimeamua katika kipindi hiki cha kumalizia masomo niweke kwanza muziki pembeni mpaka pale nitakapomaliza ili niweze kufanya vyema katika masomo maana kuchanganya mambo mawili kwa wakati mmoja ni ngumu,” alisema Bill Nas.

Leave A Reply