The House of Favourite Newspapers

Aunt Lulu, Isabela Watia Aibu Msibani Kwa Balozi Sisco

0
Isabella Mpanda.

STORI: GLADNESS MALLYA NA HAMIDA HASSAN, RISASI JUMAMOSI, HABARI

MASTAA wasioisha vituko vya aibu mjini, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ na mwenzake Isabella Mpanda hivi karibuni walitia aibu msibani kwa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Sisco Mtiro na kuwa kero kwa waombolezaji wengine.

Aunty Lulu na mwenzake walinaswa na Risasi Jumamosi wakijiachia kwa kunywa pombe nyumbani kwa balozi huyo aliyezikwa Jumatano wiki hii katika Makaburi ya Kisutu ambapo kabla ya mwili wake kupumzishwa kwenye nyumba ya milele uliagwa nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar na kuhudhuriwa na watu kibao wakiwemo watu mashuhuri.

Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’.

Mastaa hao bila aibu walikaa nyuma ya ukuta wa nyumba ya marehemu ambapo kulikuwa na kisomo cha akina mama, wakati dua ikiendelea wao w a k a w a wanakunywa huku wakipitapita mbele ya watu.

Baadhi ya waombolezaji waliokuwa eneo hilo walikerwa na tabia za mastaa hao ambapo waliishia kuwasema pembeni bila kuwakanya kwa tabia hiyo waliyoionesha.

Hata hivyo, mapaparazi wetu walizungumza na Isabella ambaye alikuwa akijionesha wazi bila kificho sababu ya kunywa hadharani wakati akiwa msibani akadai kuwa, kutokana na majonzi aliyokuwa nayo alikuwa hana jinsi zaidi ya kunywa pombe ili kuwa sawa kwani msiba huo umemuumiza sana.

“Nimekuja kumuaga kaka yangu, yaani Mmakonde mwenzangu, Sisco aliwahi kunisaidia mengi sana kwa hiyo huzuni niliyonayo imenifanya ninywe tu nilewe ili nisahau maana nimeumizwa sana na kifo chake,” alisema Isabela. Lulu alipobanwa sababu ya kuonekana amelewa vile, tena msibani alishindwa kujielezea zaidi ya kucheka kitendo kilichoendelea kuwa kero.

Leave A Reply