The House of Favourite Newspapers

BILNASS ANGEFANYA NINI KAMA SIYO MUZIKI?

Bilnass.

UNAWEZA kuwa umewahi kujiuliza kwamba, mbali na muziki, mkali wa kurap Bongo, anayefahamika zaidi kwa jina la Bilnass angefanya kazi gani au angejihusisha na shughuli gani na ukakosa jibu? Sasa Bilnass mwenyewe anakupa jibu hapahapa, sikia;

 

Akichonga na Risasi Vibes, Bilnass alisema kwamba, kama masuala ya muziki yangemwendea kombo, basi angekomaa na kitabu na kufanya kazi ya uhasibu katika makampuni makubwa ndani na nje ya nchi.

 

“Ninapenda sana masuala ya uhasibu, kucheza na mpunga (pesa). Kwa hiyo kama muziki ungeniendea kombo, ningekomaa tu na kitabu, ndiyo maana unaona hata nilichosomea ni mambo hayohayo. Kwa hiyo masuala ya pesa ndiyo kitu ninachokiinjoi maishani mwangu,” alisunguka Bilnass.

Boniphace Ngumije.

Comments are closed.