The House of Favourite Newspapers

Z Anto atamba kufuta vumbi ‘kiti’ chake

Z Anto.

HIVI jifikirie duniani kusingekuwa na muziki wa aina yoyote ile maisha yangekuwaje? Kungekuwa na raha kweli? Watu wangewatumia nini wapenzi wao mbali na muziki safi wenye maudhui ya mahaba?

Kuna makabila misibani hucheza muziki wanapowasindikiza wapendwa wao kwenye mapumziko yao ya milele, wengine muziki huwaliwaza wanapokuwa kwenye maswaibu mbalimbali. Unaweza kuwa muziki wa kidunia, wa dini au wa asili, utaukwepaje muziki?

 

Ukiwa unatafakari suala hili jiulize pia kuhusu unapokuwa na mwanamuziki unayempenda, anafanya kazi nzuri na unazifuatilia, alafu baadaye anapotea! Bila shaka ni dhahiri kuna kitu pia kinakuwa kimepungua kwa upande wako.

Kwa mantiki hiyo utakubaliana na mimi kwamba kupotea kwa mwanamuziki Z Anto, aliyetamba na nyimbo nyingi zikiwemo Binti Kiziwi, Kisiwa cha Malavidavi na Mpenzi Jini, kuna baadhi ya watu walikosa kile kitu moyo unapenda.

 

Na pengine wamekuwa wakijiuliza maswali yupo wapi? Kwa nini harudi na kushika gemu kama ilivyokuwa zamani? Na mengine mengi kuhusu yeye na kazi yake. Huyu hapa Z Anto ana majibu ya maswali yako.

Risasi: Kaka umepotea sana, tatizo nini?

Z Anto: Mbona nipo, tena hivi karibuni nimetoa ngoma kali iitwayo Nenda Kacheze Unakochezaga.

Risasi: Ni kali lakini haijakurudisha kwenye siti yako ambayo ulikuwa umeikalia awali.

 

Z Anto: Ni kweli. Muziki una changamoto nyingi.

Risasi: Changamoto zipi hizo, ndizo zilizokupoteza?

Z Anto: Changamoto za muziki ni pamoja na kuwa na menejimenti nzuri, inayoweza kusimamia kazi zako mwanzo mwisho na kuzifikisha kwa walaji ukiwa huna menejimenti kiukweli hata muziki wako hauwezi kufika mbali.

 

Kuhusu mimi kuondoka kwenye gemu, ni changamoto za hapa na pale za kimaisha na mabadiliko ya gemu. Si unajua hata mfalme hawezi kuwa mfalme siku zote. Kuna wakati unafika watu wengine wanachukua siti, lakini ile siti yangu ninarudi kuifuta vumbi.

Risasi: Kumekuwa na changamoto, wanamuziki wengi mkipotea kwenye gemu kurudi inakuwa shida, unafikiri nini kinasababisha hali hii?

Z Anto: Bila shaka baadhi ya wanamuziki wanalisoma gemu vibaya. Wanashindwa kuelewa nini kiliwapoteza kwenye gemu na kipi wanatakiwa kufanya na kurudi pale walipokuwa. Hilo ndilo linakuwa tatizo hasa. Ukiwa nje ya gemu na unahitaji kurudi unatakiwa kuhakikisha unalisoma kwelikweli, la sivyo ukirudi unaweza kuwa kichekesho.

 

Risasi: Kwa upande wako kipi unaona ukifanya kitakurudisha kule ulipokuwa?

Z Anto: Kazi nzuri zinazoendana na muda. Hicho ndicho ninachokifanya na hata ukitazama kazi yangu mpya utagundua hilo. Kwa hiyo mashabiki wangu wasiwe na wasiwasi, ni kweli walikwua wameshachoka kusubiri lakini wakati umefika wa kumpata Z Anto yule wanayemfahamu wao.

Risasi: Lakini kuna tetesi kwamba mambo ya kifamilia ndiyo yalikupoteza, ni mambo gani hayo?

Z Anto: Si kweli,nipo vizuri na familia yangu na maisha yanaendelea kama kawaida. Na kwa upande wa familia yangu sitaki kuzungumzia zaidi, tuzungumzie kazi.

 

Risasi: Mashabiki wako wategemee nini zaidi?

Z Anto: Kazi nzuri na wategemee kumpokea Z Anto mpya.

nikatofautiana nayo na ndiyo sababu hasa iliyonifikisha hapa nilipo kimuziki kwa sasa.

Risasi: Pole sana. Kwa hiyo kwa sasa unajishughulisha na nini zaidi?

Nas: Ni muziki huuhuu. Lakini katika hatua nyingine. Kwa sasa mbali na kuimba mimi ni prodyuza, ninamiliki studio yangu inayoitwa Pamoja Records. Kwa hiyo muda mwingi ninakuwa kwenye studio yangu na ndiyo inanisaidia kuendesha maisha yangu.

 

Risasi: Kuhusu muziki, una ndoto zozote pengine kama ilivyokuwa awali, au ndiyo zilikwisha futika na umebaki ukifanya kama hobi?

Nas: Ndoto zipo. Lakini ndoto huja pia kutokana na hali halisi inavyokuwa inakwenda, kwa hiyo kwa sasa ndoto zangu ni kuendeleza kwanza studio yangu ili niweze kupata studio kubwa ambayo itakuwa na nafasi ya kufanya kazi zaidi na wanamuziki wengi wa ndani na nje ya nchi.

Kisha baada ya hapo ndipo nitarudi kuangazia muziki kwa kiasi kikubwa kama ambavyo ilikuwa hapo nyuma.

 

Risasi: Ukiwa haupo kwenye ‘mainstream’, nini hasa unajifunza kutoka kwa wanamuziki wanaofanya vizuri?

Nas: Naona kuna ushindani. Ushindani ambao unaleta chachu ya watu kuzidisha juhudi na kukomaa zaidi ili waweze kufika kule ambako wanahitaji kufika kimuziki.

Risasi: Mwanamuziki gani ambaye unavutiwa naye kufanya naye kazi kwa sasa?

 

Nas: Kiukweli wapo wengi, sijaweza kumfikiria mwanamuziki mmoja kwa sasa kwa sababu sina kazi ambayo inamhusu mwanamuziki fulani. Bila shaka unafahamu kwamba si kila mwanamuziki anahitaji kumshirikisha mtu fulani, wimbo ndiyo unahitaji kumshirikisha mwanamuziki fulani.

Risasi: Una kipi cha kuwashauri wanamuziki ambao wamepotea na wanajaribu kupambana ili warudi kule walikokuwa?

 

Nas: Wasikate tamaa. Waendelee kupambana ili kuhakikisha wanafikia malengo yao. Kwa sababu muziki una kupanda na kushuka kama zilivyo biashara nyingine.

Risasi: Umefanya kazi kadhaa na 20 Percent, wewe umepotea na yeye amepotea, nini unafikiri nini sababu ya kupotea kwake?

Nas: Sijui kiukweli kuhusu 20 Percent na sihitaji kumzungumzia.

Risasi: Basi sawa ninakushukuru sana kaka, kila la kheri kwenye muziki wako.

Nas: Asante.

Makala: BONIPHACE NGUMIJE

Comments are closed.