The House of Favourite Newspapers

Binti Atupa Kitoto Kichanga cha Siku 1

0

MTOTO mchanga mwenye umri wa siku moja amekutwa amefariki dunia baada ya kutupwa kwenye kichaka na kufunikwa majani katika Kijiji cha Sagong, Kata ya Nangwa wilayani Hanan’g mkoani Manyara, huku familia ya binti anayetuhumiwa kumtupa mtoto huyo wakisema jambo hilo ni la aibu.

 

Wakizungumzia tukio hilo wanafamilia wa binti anayedaiwa kumtupa mtoto huyo wamesema kuwa hiyo ni aibu kubwa ambayo wameipata kwenye familia ikiwa ni kweli kama binti yao ambaye ametoweka kijijini hapo baada ya kufanya tukio hilo.

 

Ndugu wameongeza kwamba binti yao alikuwa na ujauzito ambao muda wa kujifungua ulikuwaumefika lakini ghafla akaonekana hana ujauzito huo tena na akatoweka nyumbani.

Leave A Reply