Yanga Kutimkia Zanzibar

KUELEKEA kutimiza mwaka mmoja wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Hussein Mwinyi, Serikali hiyo imeialika Yanga kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mafunzo au Mlandege.

 

Mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alifunguka kuwa: “Tupo kwenye maandalizi ya safari kuelekea Zanzibar kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja wa Rais Hussein Mwinyi na tumekuwa sehemu ya wageni waalikwa.

 

“Timu yetu itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mafunzo au Mlandege, ingawa Mafunzo ndiyo wapo kwenye nafasi kubwa ya kucheza na sisi.”

 

Spoti Xtra lilimtafuta Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity Kandoro ili kujua uwepo wa mchezo huo, ambapo alisema: “Safari ipo, Wanayanga watapewa taarifa rasmi muda ukifika.”

 

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa Novemba 12, huku Yanga wakitarajiwa kwenda visiwani humo Novemba 11.

r ISSA LIPONDA, DAR2173
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment