The House of Favourite Newspapers

Bobi Wine Akamatwa Polisi, Waandamanaji Wafyatuliwa Mabomu

0

MWANASIASA wa Uganda ambaye pia alikuwa mgombea urais wa chama cha upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, amekamatwa katika mji mkuu wa Kampala.

 

 

 

Wakati Bobi Wine anakamatwa, alikuwa anaongoza timu ya wabunge kutoka chama chake cha National Unity Platform, kufanya maandamano dhidi ya kukamatwa na kutoweka kwa wafuasi wa chama chake katika kipindi cha kuelekea, wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Januari.

 

 

 

Vikosi vya usalama vilifyatua vitoza machozi na kutawanya waandamaji waliokuwa wameandamana na mwanasiasa huyo. Inasemekana kwamba waliokamatwa ni pamoja na wabunge 15.

 

 

Katika mkutano uliofanyika kupitia njia ya video, Bobi Wine alitoa wito kwa wafuasi wake kutumia njia za amani kuandamana dhidi ya matokeo ya uchaguzi – ambayo anaendelea kudai kuwa vikosi vya usalama itoe wale wasiojulikana walipo.

 

 

Kukamatwa kwake kutokana na mkutano wa kampeni uliofanyika Novemba kulianza siku mbili baada ya maandamano ambapo watu zaidi ya 50 waliuawa. Gazeti la Uganda la Daily Monitor limeweka kwenye mtandao picha za Bobi Wine akikamatwa Jumatatu:

Leave A Reply