The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Filamu Yafanya Ukaguzi wa Filamu Zisizosajiliwa

0
Harakati zikiendelea kwenye maduka hayo.

Bodi ya Filamu nchini jana iliendesha zoezi la kuwasaka wafanyabiashara wanaoendesha biashara ya kuuza filamu zilisizosajiliwa na bodi hiyo.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, uliofanyika katika maduka yaliyopo mitaa ya Kariakoo jijini Dar, Afisa maendeleo ya filamu nchini, Benson Mkenda aliyemuwakilisha katibu mtendaji wa bodi hiyo, Dkt. Kiango Kilonzo amesema kuwa  moja ya kazi wanayoifanya ni  uzingatiaji wa utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ili kuona filamu zinazouzwa kama  zimepita bodi ya filam ili kuhakikiwa.

Afisa aliyeongoza zoezi hilo Benson Mkenda akizungumza na vyombo vya habari.

“Katika maduka mengi zinauzwa filamu ambazo hazina ubora haziwekwa madaraja ili kuangaliwa na watu wa rika zote.

“Filamu nyingi wanazoziuza ni  za kutoka nje ya nchi ambazo pia nazo kwa mujibu wa sheria zinatakiwa kupita bodi ya filamu ili kuhakikiwa na kupewa madaraja ili kama zinadosari katika kuangaliwa na rika tofauti ziweze kuainishwa. Ukiangalia katika maduka mengi wanachukua filamu za nje na wanazipakua mtandaoni na kuziuza bila kupeleka bodi ya filamu bila kukaguliwa, hilo ni kosa kubwa kisheria”.

Ukaguzi ukiendelea.

“Filamu kama za ila nchi ina utaratibu wake wengine wanaweza kuonyesha picha za kupigana au unyanyasaji wa kijinsia katika nchi nyingine wao zinaweza kuwa sawa lakini sisi kwetu tuna utaratibu wetu wa kusimamia sheria za jamii yetu kulingana na tamaduni zetu,”alisema Mkenda.

Mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhani akizungumza na wanahabari baada ya kunaswa.

Nae mmoja wa wawauzaji wa filamu hizoaliyenaswa kwenye zoezi hilo na kujitambulisha kwa jina la Ramadhani alisema kuwa tatizo la zoezi hilo ni kukamatwa kabla ya kuelimishwa kuhusiana na sheria hizo.

Afisa akimuonesha mfanyabiashara filamu anazouza bila kufuata utaratibu.

“Mimi ni kweli nimefanya hilo kosa lakini sijawahi kuelimshwa juu ya hayo niliyoyafanya lakini ningeelimishwa nisingefanya kwa hiyo sina la kusema wameshanikuta hapa nawasikiliza wao watakachoniambia.” Alisema Ramadhani.

Hata hivyo afisa aliyeendesha zoezi hilo (Mkenda) alisema swala la kusema hawajaelimishwa ni uongo kwakuwa wamekuwa wakiwaita ofisini kwao mara kwa mara na kuwapa elimu hiyo lakini wamekuwa wakikaidi.

Ramadhani akijaza fomu baada ya kunaswa.

Hivyo kufuatia kukiuka agizo hilo ndio maana wameamua kuwashtukiza na kuwakagua ambapo waliokutwa na makosa walipigwa faini na wasio na faini walikuwa wakitarajiwa kupelekwa mahakamani kukabiliwa na kifungo au kulipa faini hiyo.

Leave A Reply