The House of Favourite Newspapers

Tanzia: Mbunge wa CCM Afariki Dunia

0

MBUNGE  wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla, amefariki dunia katika Hospitali ya HCG Mumbai, India alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Kifo cha mbunge huyo aliyezaliwa Novemba 10, 1955 kimetangazwa leo Alhamisi Januari 21, 2021, na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ambaye amesema mbunge huyo amefariki dunia jana Jumatano Januari 20, 2021.

 

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Martha Umbulla. Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, wabunge na wananchi wa Mkoa wa Manyara. Mwenyezi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu.

 

“Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu inaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amina,” amesema Ndugai.

 

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mjini Babati, Feisal Dauda, pia amethibitisha kutokea kwa kifo hicho lakini hajaeleza chanzo cha kifo chake.

 

Umbura amekuwa mbunge zaidi ya miaka kumi ambapo hadi anafariki alikuwa Mbunge wa Viti Maalum katika mkoa huo.

 

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.

 

Leave A Reply