The House of Favourite Newspapers

Bodi ya Filamu Yawapongeza Wasanii Bongo Muvi Kuteuliwa Kuwania Tuzo Za Kimataifa

0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo (kushoto) akiwakabidhi bendera ya taifa wasanii hao kutoka kushoto, Gynah, Cojack Chilo na Ram Ally.

 

 

 

BODI ya Filamu imewapongeza wasanii wa Bongo Muvi kwa kufanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za filamu za kimataifa za Like international Pan African Film Festival kupitia Filamu ya Nyara na Mulasi tuzo zinazotarajiwa kufanyika nchini Nairobi Kenya Novemba 3  hadi 6, 202.

Mkutano huo ukiendelea.

 

 

 

Akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa kukabidhi bendera wasanii hao, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Bodi ya Filamu, Dkt Kiagho Kilonzo, amewapongeza na kuwataka watanzania kuwaombea waweze kurudi na tunzo.

Gynah akiwaomba Watanzania wamuombee kwa Mungu ili atwae tuzo hiyo.

 

 

 

“Filamu ya Nyara ambayo imefanya vizuri na imefanikiwa kushinda tuzo ya Zanzibar Internationa Filam Festival ZIFF kama filamu bora na sasa inaenda kushindana nchini Kenya kama filamu bora na mwigizaji bora wa kiume anawania Cojack Chilo.

Cojack Chilo akieleza sababu zilizomfanya kuteuliwa kuwania tuzo hizo.

 

 

 

Pia filamu ya Mulasi imeingia kama filamu bora na Mwigizaji bora wa kike anawania tuzo ni Rejina Kihwele, ‘Gynah’ anawania na wasanii kutoka nchini Afrika kusini, Cameroon na Uganda.

 

 

Aidha ameongeza kuwa serikali imeanza kutoa udhamini kwa waandaaji wa filamu wanatakiwa kuandaa  zenye maadili na kuangalia mira na desturi ya mwafrika na sio kuiga ughaibuni.

 

Kwa upande wake msanii Regina Kihwele, ambaye ameteuliwa kuingia kwenye kinyang’anyilo cha msanii bora wa kike amesema kuwa niwakati wa Tanzania kuonyesha uwezo wetu kimataifa.

 

Naye Cojack Chilo ameingia kwenye kinyang’anyilo cha filamu bora ya Nyara na kugombea msanii bora wa kiume kupitia filamu ya Nyara ambayo imefanya vizuri zaidi.

Leave A Reply