The House of Favourite Newspapers

Nabi Awapa Maagizo Maalum Aucho, Bangala

0

 

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, kweli anazitaka pointi tatu za Azam FC baada ya kuwataka viungo wake, Khalid Aucho na Yannick Bangala kupiga pasi nyingi za haraka kwenda katika goli la wapinzani.

 

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Akizungumza na Spoti Xtra, kwa
niaba ya Kocha Nabi, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze, alisema wao
benchi la ufundi wanataka kuona
timu inacheza soka la kisasa la pasi nyingi kwa lengo la kuwapa burudani
mashabiki wao.


Kaze alisema kuwa, anafurahia
kuona timu yao ikiendelea kupata matokeo mazuri ya ushindi huku
akiwazuia wachezaji wake kubutua
mipira katika michezo yao.


Aliongeza kuwa, benchi lao
la ufundi likiwa linaendelea kutengeneza muunganiko, wanataka kuona viungo Aucho, Bangala na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wakitimiza majukumu yao ya kuchezesha timu na kupiga pasi za uhakika za kuzaa mabao.


“Katika michezo ambayo
tumecheza ya ligi, timu imeonekana ikitengeneza nafasi nyingi za kufunga, pongezi nyingi ziende kwa viungo ambao wanatimiza vema majukumu yao.


“Kilichobakia hivi sasa ni kuona
viungo wakituliza mashambulizi kwa kupiga pasi nyingi za haraka huku wakiendelea kushambulia goli la wapinzani katika michezo ijayo ukiwemo dhidi ya Azam.

 

Mchezo wetu dhidi ya Azam siyo mdogo ni mkubwa kutokana na ubora wa timu yao, lakini kikubwa kama makocha tunataka kuona wachezaji wetu wanafanyia kazi mafunzo na maelekezo yetu tuliyokuwa tunaendelea kuwapa,” alisema Kaze.

Leave A Reply