The House of Favourite Newspapers

Bondia Hasaan Mwakinyo na Mpinzani Wake Liam Smith Raia wa Uingereza Wamepima Uzito

0

TAYARI bondia Hasaan Mwakinyo na mpinzani wake Liam Smith raia wa Uingereza wamepima uzito muda mfupi uliopita katika Hoteli ya Hilton kwenye Jiji la Liverpool kabla ya kesho kupanda ulingoni.

Mwakinyo na Smith watapanda ulingoni kesho Jumamosi kwenye Ukumbi wa M&S Bank Arena uliopo kwenye Jiji la Liverpool nchini Uingereza.

Pambano ambalo litapigwa kwa raundi 12 katika uzani wa Super Walter litazamiwa kuanza majira ya saa 12 za jioni kwa saa za Tanzania.

Leave A Reply