The House of Favourite Newspapers

Bonge la Nyau: Naogopa Uhusiano na Mastaa

STORI: Boniface Ngumije | UWAZI | ShowBiz

MWANAMUZIKI anayekimbiza kwenye gemu na ngoma za Vais Vesa na Aza, Bonge la Nyau amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anaogopa ni kutoka kimapenzi na mwanamke ambaye ni maarufu kwani wanakuwa na changamoto nyingi.

Bonge la Nyau

Akipiga stori na Uwazi Showbiz, Bonge la Nyau aliongeza kuwa, japo anaogopa lakini haimaanishi kuwa hawezi kuwa na staa kimapenzi pale inapotokea akampenda lakini kikubwa anakuwa naye kwa tahadhari.

“Naogopa sana kuwa kwenye uhusiano na wanawake mastaa, unajua mastaa wanakuwa na changamoto nyingi sana, kwa hiyo ikitokea nikawa naye nitajitahidi kuwa makini zaidi kukabiliana na changamoto zao maana pia watu wengi wanakuwa wanawapenda,” alimaliza Bonge la Nyau.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Comments are closed.