The House of Favourite Newspapers

Kitambi kwa Wanaume / Wanawake na Jinsi ya Kuondoa

UWAZI | AFYA

MAFUTA ya tumbo yanayofanya mtu kuwa na kitambi ambacho hukusanywa kwa njia kuu mbili:

Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI

Sababu kubwa ya mtu kuwa na kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu (kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayosababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA VINAVYOCHANGIA KULETA KITAMBI

Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na vile vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu, nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta maarufu kama chips pamoja na pizza.

Vingine ni vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi uliokobolewa, mihogo, wali, mkate mweupe na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyoongezwa kama vile soda, vyakula vilivyo tengenezwa kwa ngano na sukari kama vile keki, skonzi, chapati, maandazi na kadhalika.

Lakini pia vinywaji vilivyotengenezwa kwa kutumia ngano kama vile bia za aina mbalimbali.

Vyakula hivyo vikitumiwa bila kuzingatia kanuni za mlo kamili, huchangia kuleta kitambi.

Lakini pia kutofanya mazoezi ya viungo husababisha mtu kuwa na kitambi.

Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya vipimo vya kiuno (waist) na nyonga (hips).

Mzingo wa kiuno ukiwa 102 cm au 40 kwa wanaume na 88 cm au 35 kwa wanawake, huyo ana kitambi.

Kipimo kingine ni Body Volume Index, kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.

Tumekwisha ona hapo juu jinsi kitambi kinavyopatikana na vyakula pamoja na sababu nyingine zinazosababisha kutokea kwa kitambi, sasa tutazame mambo yatakayokufanya uwe katika hatari ya kupata kitambi.

Mambo yafuatayo huwaweka watu katika hatari kubwa ya kupata kitambi:

Ulaji mbovu wa chakula; ni ulaji usio zingatia kanuni za mlo kamili. Hapa mtu hufululiza kutumia chakula cha aina moja bila kuzingatia aina nyinginezo. Mfano; mtu anaweza kuwa anakula mlo ufuatao:

Asubuhi: Mchemsho au supu ya ng’ombe au mbuzi na chapati mbili na soda. Mchana, ugali nyama choma, anashushia kwa maji na soda.

Jioni: Mchemsho wa kuku, ulimi, mbuzi na bia.

Usiku: Chips mayai au chips kuku au chips mishikaki na bia au soda.

Mtu huyu akiendelea na utaratibu huu kwa muda mrefu, ni lazima atakuwa na kitambi.

Kwa hiyo ulaji mfululizo wa vyakula vyenye mafuta mengi, sukari iliyoongezwa (added sugar), vyakula vya ngano na kutofanya mazoezi ya mwili na viungo ( physical exercises), huchangia mtu kuwa na kitambi.

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI

Kuwa na kitambi maana yake una mafuta yasiyohitajika mwilini, mwili wako unatumika kuhifadhi mafuta hayo. Hali hii ina maana kuwa ogani nyinginezo zilizomo ndani ya mwili wako zinaogelea kwenye mafuta yasiyohitajika ndani ya mwili wako, ja mbo ambalo ni hatari kubwa ya kushambuliwa na magonjwa hatari kama vile shinikizo kubwa la damu, kiharusi na kisukari na kwa kutaja machache.

Hivyo basi ili kuondokana na hatari hiyo, yakupasa kupambana kuondoa hayo mafuta yasiyohitajika mwilini mwako.

NJIA ZA KUONDOA KITAMBI

Unaweza kuondokana na kitambi kwa kufanya diet pamoja na mazoezi ya mwili na viungo.

Vilevile unaweza kuondoa kitambi na kupunguza mafuta mwilini kwa kutumia dawa asilia au za kizungu za kuondoa kitambi na kuondoa mafuta yasiyohitajika mwilini.

Kwa stori zote kali, Tu-follow

Facebook @Globalpublishers

Twitter @GlobalHabari

Instagram @GlobalPublishers

YouTube @GlobalTVTZ

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Save

Comments are closed.