The House of Favourite Newspapers

Bongo Movies wafungua Tawi la Yanga

0

mike sanguMike Sangu

Na Hamida Hassan,  Dar es Salaam

MASTAA wa Bongo Movies wanaoshabikia Timu ya Yanga wamefungua tawi rasmi kwa ajili ya kuisapoti hiyo ya Jangwani.

Yanga imekuwa na mashabiki wengi kila kona hapa nchini na Bongo Movies wameanzisha tawi hilo ili kuwa karibu zaidi na timu hiyo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa tawi hilo, Mike Sangu, baada ya kuona wanajitosheleza kufungua tawi lao waliamua kukutana na kuhimizana kufungua tawi pamoja na kuchagua viongozi mbalimbali.

“Tulipokubaliana tuliongea na Jerry Muro (ofisa habari wa Yanga) ambaye alitusaidia kupata usajili na sasa tunatambulika rasmi,” alisema Mike.

Aliwataja wasanii wengine wanaounda tawi hilo ambao wote ni wachezaji filamu kuwa ni, Wema Sepetu, Baby Madaha, Isabela Mpanda, Miriam Jolwa ‘Kabula’, Halima Yahaya ‘Davina’, Esha Buheti, Flora Mvungi, Jimmy Mafufu, Jack Pentizel, Mayasa Mrisho, Catherine Ambakisye ‘Mama Rolaa’, Sauda Mwilima, Hassan Moshi, Sabrina Rupia ‘Cathy’, Mary Mawigi, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine wengi.

Leave A Reply