The House of Favourite Newspapers

Alicia Keys Apinga Matumizi Ya Make Up

0

alicia-keys-2015-billboard-women-in-music-event-in-new-york-city_1 Milan, Italia

MWANAMUZIKI Alicia Keys ameendeleza mpango wake wa kupinga matumizi ya make up baada ya kupanda jukwaani kwenye shoo aliyoifanya Che Tempo che Fa mjini Milan akiwa ‘necheroo’.

Alicia amekuwa akizipinga make up ili kuwashawishi wanawake wote duniani kujikubali jinsi walivyo na kuukubali urembo waliopewa na Muumba.

Alicia-Keys-to-release-new-album-in-2015Mashabiki wa staa huyo walisema kuwa wanafurahishwa na muonekano wake na wanampongeza kwa hatua yake ya kupinga matumizi ya make up kwani ni wanawake wachache duniani hasa mastaa wenye uwezo wa kufanya hivyo.

“Wengi wao wanapenda sana ‘make up’, kutoka kwenda kwenye shoo bila ya kujiremba wanaona hawajakamilika, Alicia anaonekana mrembo zaidi pamoja na kuvaa kilemba na kutopaka chochote usoni mwake,” alisema shabiki mmoja alipoziona picha zake mtandaoni.

Alicia alizindua kampeni yake inayoitwa ‘No Make Up’ hivi karibuni ambapo wapo waliompongeza lakini wapo waliomponda na kudai kuwa yeye anapendeza bila make up kwa sababu ana ngozi nzuri na sura yake ina mvuto si kama wengine ambao wakiacha atakuwa amewaponza.

Leave A Reply