The House of Favourite Newspapers

Hatua ya Kihistoria, Bongo Muvi Sasa Kushiriki Tuzo za Oscars Nchini Marekani

0
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. Kiagho Kilonzo (kushoto) na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt. Mona Mwakalinga walipokuwa wakizungumza na wanahabari kuhusiana na neema hiyo kwa Bongo Muvi.                                                                                                                                                                                           

TASNIA ya filamu nchini yazidi kupiga hatua ya kihistoria ambapo katika mafanikio hayo kimataifa, Bodi ya Filamu imepata fursa ya kushirikisha filamu za hapa nchini kwenye tuzo zenye heshima kubwa ulimwengu za Oscars. Hayo ni mafanikio makubwa ya kihistoria hapa nchini imeelezwa na wadau.

 

Akizungumza na wanahabari Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Dkt. Kiagho Kilonzo amesema bodi ilipendekeza majina ya wadau kutoka kada mbalimbali zinazohusiana na tasnia ya filamu kwenda kwenye Academy ya Oscars kwa lengo la kuunda kamati rasmi ya kitaifa ya kuchagua filamu ya Oscars.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Dkt. Kiagho Kilonzo (mwenye suti) akiwa na kamati ya maandalizi.

 

Amesema mchakato huo ulianza mwaka 2019 baada ya uchunguzi na kujiridhisha Oscars Academy iliipitisha rasmi kamati hii mnamo Juni 30 mwaka huu. Dkt. Kilonzo ameendelea kusema kuwa kamati hii inaundwa na wajumbe 10 ambao ni Dkt. Mona Mwakalinga ambaye ni mwenyekiti wa kamati hii Simon Peter (Katibu), Profesa Martin Mhando , Single Mtambalike, Binay Gokani, Zamaradi Nzowa, Adam Juma, Daniel Manege, Florence Mkinga  na Yvonne Cherie.

 

Ameendelea kusema Dkt. Kilonzo kuwa kamati hii itakuwa na majukumu ya kupokea na kuchuja filamu zitakazokuwa zikiwasilishwa na watayarishaji ili kupata filamu moja ndefu na iliyokidhi vigezo vyote ambayo itawasilishwa kwa waendeshaji wa tuzo hizo nchini Marekani.

 

“Hivyo basi napenda kusema kuwa kamati hii ya kuchagua Filamu ya Oscars Tanzania inatoa wito kwa watayarishaji wa filamu kuwasilisha filamu zao kwa ajili ya kuzishirikisha kuwania Tuzo za 95 za Oscars.

 

“Kwa mdau yeyote anayetaka kujua zaidi kuhusiana na mchakato mzima wa kufanya ili kushiriki mchakato huu aingine kwenye mitandao yetu ya kijamii kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi. Kamati hii itaanza kupokea filamu hizo kuanzia Agosti 1 mwaka huu mpaka Agosti 30 mwaka huu ambapo link za filamu hizo kupitia barua pepe ya [email protected]” Alimaliza kusema Dkt. Kilonzo.

Leave A Reply