The House of Favourite Newspapers

Kim Jong-Un Asema Korea Kaskazini Iko Tayari Kuhamasisha Vikosi Vya Nyuklia

0
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un

RAIS wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un amesema kuwa Korea Kaskazini iko tayari kuhamasisha vikosi vyake vya Nyuklia kupambana na nchi yoyote itakayo onekana inatishia usalama wan chi hiyo, Kim ameyasema hayo katika hafla ya kuazimisha vita vya Korea.

 

Akizungumza katika hafla ya kuazimisha Vita hiyo, Rais Kim amenukuliwa akisema kwamba nchi hiyo iko tayari kabisa kwa makabiliano yoyote na Marekani.

 

Shirika la Habari la Serilkali (KCNA) liliripoti habari hizo na kudai kuwa Kumekuwa na wasiwasi kwamba Korea Kaskazini inaweza kuwa inatayarisha jaribio la saba la Nyuklia.

 

Marekani ilionya mwezi uliopita kuwa Pyongyang inaweza kufanya jaribio hilo wakati wowote, jaribio la hivi majuzi la Korea Kaskazini lilifanywa mwaka 2017, Hata hivyo hali ya wasiwasi imekuwa ikiongezeka kwenye Rasi ya Korea.

Wanajeshi wa Korea Kaskazini wakisikiliza Hotuba ya Rais wa nchi hiyo Kim Jong Un

Mwakilishi Maalum wa Marekani nchini Korea Kaskazini Sung Kim, amesema Korea Kaskazini imefanya majaribio kwa idadi isiyokuwa ya kawaida ya Makombora Mwaka huu ambayo ni jumla ya makombora 32 tayari yameshafyatuliwa ikilinganishwa na Makombora 25 katika mwaka 2019 ambapo ilivunja rekodi.

 

Mnamo mwezi Juni mwaka huu, Korea Kusini ilijibu kwa kurusha Makombora yake nane.

Leave A Reply