The House of Favourite Newspapers

BOOMPLAY YAJA NA SHAVU KWA WASANII

Natasha Stambuli General Manager wa Boom Play Tanzania

Kampuni ya Boom Play Tanzania inayodili na kusambaza muziki imekuja na shavu kwa wasanii wa Bongo kwa kuwaletea mfumo wa mtandao ili kuwasaidia kuuza muziki wao na kupata kipato.

 

Akizungumza na Global Publishers, Meneja wa Boomplay Tanzania, Nataka Stambuli alisema mfumo huo utawapa nafasi wasanii wa muziki kujitengeneza kwa kupeleka nyimbo zao kwa ajili ya kusambazwa nchi nyingi duniani.

 

“Tumewapa wasanii platform ya kufanya muziki wao na kuji-brand kisha kuleta muziki wao kwetu na sisi tutausambaza kwa wateja.

 

“Pia msanii atanufaika kupitia wateja wanavyonunua kupitia mtandao.
“Si kwamba tunachagua, msanii yeyote ambaye anafanya kazi yake vizuri tutaichukua na kuisambaza.
“Kwa sasa tupo katika nchi nne yaani Kenya, Nigeria, Tanzani na Ghana na siku zijazo tutazidi kusambaza nchi mbalimbali.

 

“Pia tutawatembelea kuwapa elimu wasanii wote wakiwemo wa mikoani hata sehemu kama Mbagala ambapo hata mtu anayeishi mazingira hayo, awe anapakua kupitia Boomplay ili kuweza kumnufaisha msanii,” alisema.

            Msanii G Nako nae alikuepo katika  tukio hilo la kutoa elimu kwa wasanii

 

Kwa upande wake, msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ wa Kundi la Navy Kenzo aliipongeza Boomplay kwa kuwa imewapa nafasi na sasa ameona matunda.

Msanii wa Bongo Fleva Nahreel wa Kundi la Navy Kenzo aliipongeza Boomplay

“Mimi nilijiunga na Boomplay na kipindi ambacho nilijiunga, kama unavyojua kuna wenzetu walikuwa wakisema tutadhulumiwa, lakini nilisema acha niingie nijue nini ambacho kitanitokea.
“Nilipeleka muziki wangu na kwa bahati nzuri, soko likawa limekua sana.

“Nimepata mafaniko makubwa hivyo ninawasii wasanii wenzangu waji-brand maana kama wewe ni msanii wa muziki wa Asili kama Mrisho Mpoto, basi jitahidi muonekano wako uwe wa kiasili kisha peleka nyimbo zako Boomplay, alisema Nahreel.

Msanii wakazi akitoa maoni


Katika tukio hilo la kutoa elimu kwa wasanii katika Hoteli ya Coral Beach iliyopo Masaki jijini Dar walikuwepo wasanii kibao kama Wakazi, G Nako, Cpwa na wengineo.

Stori: Neema Adrian, Global Publishers

Comments are closed.