The House of Favourite Newspapers

Bosi Simba Atoa Tamko Nzito, Afanya Kikao Kizito na Wachezaji

0
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’ (katikati) akiongea jambo.

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’ amefunguka kuwa, kwa sasa wanakwenda kwenye ukurasa mpya na klabu hiyo.

Juzi Jumapili, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba pamoja na wachezaji wa timu hiyo, walifanya kikao cha takribani siku nzima, lengo likiwa ni kufahamu changamoto zilizopo ambazo huenda zinasababisha wapitie kwenye kipindi kigumu kwa sasa.

Kikao hicho kiliongozwa na Try Again na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika kikao hicho, muafaka umepatikana wa kuyafikia malengo yao waliyoyalenga msimu huu.

Kwenye kikao hicho, wachezaji wa Simba waliahidi kuipambania nembo ya klabu hiyo, pamoja na kuyafikia malengo ambayo ni kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, sambamba na kurejesha furaha kwa mashabiki wao.

Kikao hicho kimeamua kutengeneza ukurasa mpya baada ya magumu ambayo wamepitia Simba ndani ya michezo mitatu iliyopita. Ikiwemo kula chuma 5-1 mbele ya Yanga, sare ya 1-1 na Namungo, kisha sare ya 1-1 na ASEC Mimosas kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Baada ya kikao hicho, Try Again aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram akisema: “Ukurasa Mpya.”

Moja ya Wajumbe wa Bodi ya Simba ambaye aliomba hifadhi ya jina lake, alisema: “Kauli ya mwenyekiti wetu ina maana kubwa sana, sasa tunakwenda kufanya makubwa na timu yetu imefungua ukurasa mpya wa kuyafikia malengo yetu.”

ANAYEDAI KUTESWA ADAI MIL 500 KWA MBUNGE GEKUL WAMALIZANE, MAHAKAMANI IJUMAA, WAKILI MADEREKA ANENA

Leave A Reply