The House of Favourite Newspapers

Bosi Simba: Matola Haendi Popote

0

OFISA Mtendaji Mkuu wa Simba (C.E.O), Senzo Mazingisa, amesema kuwa kocha msaidizi wa timu hiyo, Selemani Matola, bado yupoyupo sana katika kikosi cha timu hiyo, wala hana mpango wa kuondoka.

 

Kauli hiyo imekuja mara baada ya kuibuka kwa tetesi zikimhusu Matola kutakiwa na klabu ya Azam FC kwa ajili ya kuwa kocha msaidizi katika kikosi chao.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Senzo alisema kuwa anaamini kocha huyo ana furaha kubwa ndani ya kikosi cha Simba ambacho ni mabingwa wa ligi kuu, hivyo kama angehitaji kuondoka uongozi ungefahamu kwa kuwa bado ana mkataba wa kuitumikia Simba.

 

“Matola ana furaha kuwepo Simba, ameifanikisha timu kuwa bingwa wa ligi msimu huu, akiwa kama kocha msaidizi, sasa nashangaa kuona kuwa wanasema ataondoka wakati bado ana mkataba na sisi.

 

“Kama ambavyo unafahamu kwa mtu mwenye mkataba kumchukua lazima uvunje mkataba, sasa wao watavunjaje mkataba kama hawajazungumza na sisi Simba? Labda kama watakuja lakini kwa sasa hakuna taarifa wala mazungumzo juu ya kuodoka kwa Matola,” alisema bosi huyo.

STORI: MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

Leave A Reply