The House of Favourite Newspapers

Bosi wa Manchester City Atangaza Kikao Na Mastaa Wake Kufanya Uamuzi

0
Pep Guardiola

BOSI wa Manchester City, Pep Guardiola, amesema atakaa na wachezaji wake kabla ya kufanya uamuzi ambao kwake anaona utakuwa sahihi.

Hii ni katika kuelekea mwishoni mwa msimu ambapo Man City imepanga kuzungumza na nyota wake kabla ya kupeana mkono wa kwaheri.

Guardiola amepanga kuzungumza na wachezaji wake kama kuna ambao wanahitaji muda zaidi wa kucheza au wanataka kuondoka, hayo yote yatafahamika mwishoni mwa msimu huu.

Mpaka sasa kuna tetesi kuwa, huenda Man City ikamuuza kiungo wake Kalvin Phillips ambaye ameshindwa kuonesha cheche zake ndani ya kikosi hicho tangu asajiliwe.

Guardiola alisema kwa sasa ni bora wakaendelea kupambana kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa na msimu utakapomalizika watazungumza.

“Mwisho wa msimu ukifika tutakaa na wachezaji wote na kujadili mambo kadhaa juu yao na klabu.

“Huenda kuna wengine wanahitaji dakika zaidi za kucheza au wengine hawana furaha kuwa hapa. Hivyo tunasubiri muda huo ukifika kila kitu kitajulikana.

“Kwa sasa siwezi kuzungumzq chochote ila wachezaji wangu wote ni muhimu katika timu hii, hilo lieleweke,” alisema Guardiola.

RASMI! HARMONIZE AMTAMBULISHA MPENZI MPYA ‘MRWANDA’, KAJALA ASHINDWA KUJIZUIA, AMPIGA DONGO..

Leave A Reply