The House of Favourite Newspapers

Breaking: Hatimaye Sumaye Arejea CCM

0

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye,  leo Februari. 10, 2020, ametangaza kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM). Desemba 4, 2019, Sumaye alitangaza kuachana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akidai kuwa hakuna demokrasia ndani ya chama hicho baada ya kushindwa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani.

 

Sumaye aliondoka CCM na kujiunga CHADEMA Agosti 22, 2015 wakati wa uchaguzi mkuu kwa alichokiita malengo ya kuimarisha upinzani na sasa ametangaza uamuzi wa kurejea CCM katika Kikao cha Baraza la Wadhamini, Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba – Dar es Salaam.

 

”Nilikwenda kujenga upinzani, ila kwa nilichokikuta huko, kazi kubwa ni kupambana na polisi na usalama wa Taifa hawana ajenda nyingine, hakuna upinzani dhahiri ni upinzania maslahi.

 

”Naomba mnipokee ndugu zangu na ninaahidi kushirikiana kwa moyo mkunjufu na Watanzania wananijua huwa sina unafiki. Baada ya kuhangaika na hawa jamaa zangu, nikaona kwa kweli nabeba maji kwa gunia, faida pekee ni kuloana mgongo tu,”  amesema.

Leave A Reply