BREAKING: JPM Aanika Sababu za Kuwabadilisha Kabudi na Mahiga – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli, leo Machi 04, amewaapisha Balozi Dk. Augustine Phillip Mahiga kuwa Waziri wa Katiba na Sheria na Prof. Palamagamba John Mwaluko Aidan Kabudi kuwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 

Akihutubia mara baada ya kuwaapisha mawaziri hao, Magufuli amesema;

“Mengi yamezungumzwa, na Mimi niungane na wengine kuwapongeza wote mlioapishwa. Nimefanya mabadiliko haya kwa sababu za kawaida, ukiwa kocha unaweza kubadilisha wachezaji wako. Wako wanaosema huyu sio Mwanasheria, kwani anakwenda kufundisha Sheria?

“Wizara ya Sheria imejaa wanasheria, sasa unaweza kumpeleka Mwanadiplomasia ili akaweke mambo sawa. Naamini Watu wa Wizara ya Mambo ya Nje watampa ushirikiano. Kwenye Wizara ya Mambo ya Nje, nako kunahitaji mtu kama Prof. Kabudi ili aende akawasukume. Ukichanganya Sheria na Diplomasia mambo yanakuwa mazuri. Prof. Kabudi ni muwazi sana,” amesema Magufuli.

VIDEO: FUATILIA TUKIO LOTE HAPA

Toa comment