The House of Favourite Newspapers

BREAKING: Majaliwa Awasili Msibani kwa Mama wa Eric Shigongo – Video

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Global GroupEric James Shigongo,  marehemu Bi. Asteria Kahabi Kapela aliyefariki dunia leo kwa ajili ya kutoa pole kwa wanafamilia kwa kuondokewa na mama yao.

 

Bi. Kapela amefariki dunia alfajiri ya leo IjumaaJulai 27, 2018 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya KikweteMuhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ambapo msiba huo upo nyumbani kwa marehemu maeneo ya Mikocheni B jijini Dar es Salaam ambako taratibu zote za mazishi zitafanyika.

 

Mwili wa marehemu Asteria Kapela unatarajiwa kuagwa Jumatatu na kusafirishwa kwenda nyumbani Mwanza na mazishi yatakayofanyika Jumatano ijayo.

 

Bwana alitoa na Bwana Ametwaa, jina lake lihimidiwe, AMEN!

 

BREAKING: Majaliwa Awasili Msibani kwa Mama wa Eric Shigongo

Comments are closed.